KITAULO CHA MANULA CHAZUA ZOGO KENYA

KITAULO CHA MANULA CHAZUA ZOGO KENYA

8953
0
KUSHIRIKI

NA ALLY KAMWE

KITENDO cha marefa kumlazimisha kipa wa Simba, Aishi Manula,  kukiondoa kitaulo chake wakati wa penalti kimemkera kipa huyo akiwaomba waandaaji wa  mashindano ya SportPesa, kusemea ishu hiyo.

Marefa wamekuwa wakimlazimsha Manula kuondoka taulo lake la kufutia jasho  ilipofikia hatua ya kupigiana penalti katika michezo miwili iliyopita.

“Nawaomba waandaaji  wa mashindano  hii walifanyie kazi maana haiwezekani ndani ya dakika 90 waruhusu , lakini tatizo lije kwenye penalti.

 Manula amewatoa hofu mashabiki wa Simba na Watanzania kwa kusema kuwa yuko fiti na atacheza mchezo wa fainali.

 “Huku tuko makipa wawili tu,  hivyo ni lazima nijikaze na nipambane kuhakikisha nacheza mchezo wa fainali na kuisaidia timu yangu kubeba kombe,”  alisema Manula

Katika hatua nyingine beki wa timu hiyo Shomar Kapombe, amesema miili i ya Gor Mahia haiwatishi.

Kapombe alisema anafahamu kuwa wachezaji wa Gor Mahia wana miili mikubwa,  lakini hilo haliwatishi kwani lengo lao ni kuifunga timu hiyo na kubeba taji.

 “Gor Mahia wanacheza soka la chini na nguvu na hii ni kwa sababu ya kuwa na wachezaji wenye nguvu lakini hilo halitupi shida. Sisi tumeshacheza mechi nyingi na wachezaji tofauti tofauti hivyo tuna uzoefu wa kutosha wa kushinda ,”alisema.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU