Hasira za Van Gaal zamchekesha Martial

Hasira za Van Gaal zamchekesha Martial

470
0
KUSHIRIKI

Anthony-Martial-608483LONDON, England

STRAIKA wa Manchester United, Anthony Martial, amekiri akisema kuwa hasira zinazooneshwa na kocha wake, Louis van Gaal, zinamfanya acheke.

Martial, ambaye anakipiga katika timu ya Taifa ya Ufaransa, amekuwa kwenye kiwango kizuri tangu alipojiunga na timu hiyo Septemba, mwaka jana, kwa ada ya pauni milioni 36 akitokea katika timu ya Monaco, baada ya kufunga mabao 12 katika mashindano yote.

Kiwango hicho kizuri cha Martial kinaonekana kuwavutia wengi, akiwamo Van Gaal, lakini nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 anasema kuwa hasira zinazooneshwa huwa hazimkai rohoni.

“Huwa ananiwakia,” Martial aliuambia mtandao wa RTL. “Lakini huwa inanifanya nicheke kwa sababu nafahamu ubora wangu,” aliongeza nyota huyo.

Kwa sasa Man United bado inafukuzia nafasi ya kufuzu kucheza kwenye michuano ya Klabu Bingwa Ulaya ikiwa kwenye nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu, ikiwa ni pointi moja nyuma ya timu inayoshika nafasi ya nne, Manchester City.

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU