INAKERA

INAKERA

209
0
KUSHIRIKI

wenger-cropped_1r8n8o6nhzr1f1dkwq20wqn8u0Seaman amkingia kifua Wenger

LONDON, England

KWA kile unachoweza kusema ni kama amesema inakera, nyota wa zamani Arsenal, David Seaman, amesema kwamba amechoshwa na mtazamo hasi dhidi ya kocha wa timu hiyo, Arsene Wenger na ameonya kuwa mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi endapo Mfaransa huyo atafukuzwa.

Wenger alitimiza miaka 20 Arsenal Oktoba 2015, lakini wiki za hivi karibuni amejikuta akiwa amekaliwa kooni, baada ya Gunners kushindwa kuendeleza kasi yao katika mbio za Ligi Kuu na kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la FA.

Hata hivyo, pamoja na matokeo hayo mabaya, Seaman anaamini bado Mfaransa huyo ni mtu sahihi kuendelea kubaki kuinoa klabu hiyo ya Emirates.

“Nimechoshwa sana na habari za mtazamo hasi kuhusu Arsenal,” Seaman aliliambia gazeti la Sunday Mirror toleo la jana.

“Mabadiliko ya kocha? Kwangu hapana. Mimi ni shabiki mkubwa wa Arsene.

“Subiri tuone nini kitatokea mwisho wa msimu huu. Tuone nini kimekwenda tofauti tuweze kusahihisha. Kwangu mimi, mambo yapo sawa kabisa,” alisema kinara huyo wa zamani.

Alisema kwamba, amewahi kufanya kazi naye kwa muda wa miaka saba au nane na alikuwa mtu safi sana, huku akisema kuwa yupo upande wa Arsene na akasema kuwa daima amekuwa akisema hivyo na hana sababu ya kubadili akili yake.

“Hebu itazame Manchester United. Angalia kile kinachowatokea. Wamemkosa kocha mahiri Alex Ferguson. Hali utaiona nzuri kwa klabu nyingine.”

Seaman anaelewa hasira za mashabiki wa Arsenal, lakini amewataka kubaki na mtazamo chanya na kuendelea kuwa na matumaini katika mbio za ubingwa.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU