Msami naye achorwa tattoo

Msami naye achorwa tattoo

1289
0
KUSHIRIKI

Msami GiovaniSTAILI ya wasanii kuchorwa tattoo na wapenzi wao inazidi kushika kasi ambapo kwa sasa dansa Msami Giovani, naye amechorwa tattoo na mpenzi wake.

Msami ambaye awali alikuwa na mahusiano na msanii wa Bongo Movies, Irene Uwoya na baadaye kuachana naye sasa amepata mpenzi mwingine ambaye ameonyesha mapenzi kwa kumchora tattoo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Msami alisema anamheshimu sana mrembo huyo ambaye ameonyesha mapenzi.

“Siwezi kusema lolote kwa sasa ila namshukuru sana kwa mapenzi haya aliyonionyesha nikiongea sana nitaharibu,” alisema.

Katika hatua nyingine, Msami alitoa shukrani kwa menejimenti yake baada ya kumnunulia gari aina ya  Toyota Ipsum yenye thamani ya Sh milioni 15.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU