Linex, Christian Bella waileta Hewala

Linex, Christian Bella waileta Hewala

643
0
KUSHIRIKI

LinexNA CHRISTOPHER MSEKENA

BAADA  ya kufanya vizuri na wimbo wake unaoitwa Kwa Hela, msanii wa miondoko ya Bongo Fleva, Sunday Mangu ‘Linex’, leo anatarajia kuachia wimbo alioupachika jina la Hewala akiwa amemshirikisha Christian Bella.

Linex, ameliambia Papaso la Burudani, kuwa sababu kubwa iliyomfanya amshirikishe Christian Bella ni mfanano wao wa kutumia sauti kwa kuwa yeye anaitwa Voice Of Africa (VoA) huku Bela akiitwa The Best Melody.

“Wimbo rasmi unaachiwa kesho (leo). Bella ni msanii mkubwa na sababu nyingine iliyofanya nimshirikishe yeye ni kuwapa burudani ya mziki mzuri mashabiki kufuatia uwezo wetu wa sauti, Dansi na Bongo fleva ikikutana lazima muziki mzuri utoke,” alisema Linex.

Aliongeza kuwa baada ya leo kuiachia audio ya wimbo huo wiki ijayo video ya Hewala itakuwa mtaani hivyo mashabiki wateendelea kuipata burudani ya muziki wake.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU