Balotelli kula ‘dili’ China

Balotelli kula ‘dili’ China

372
0
KUSHIRIKI
Mario Balotelli

LONDON, England

STRAIKA Mario Balotelli anaripotiwa kuwa mbioni kuondoka katika klabu yake ya Liverpool ili akakipige nchini China.

Kwa mujibu wa gazeti la Corriere della Sera, wakala wa Balotelli aliwahi kufanya mawasiliano na klabu za China tangu Januari mwaka huu, wakati straika huyo akitafuta mahali pa kucheza kwenye kikosi cha kwanza msimu ujao.

Gazeti hilo liliripoti kuwa taarifa hizo zinaweza kuwa nzuri kwa Reds, ambao wanahangaika kumuuza nyota huyo tangu aliporejea kwenye kikosi hicho baada ya kumaliza kukipiga kwa mkopo AC Milan.

Liverpool ilitumia pauni milioni 16 kumnunua staa huyo raia wa Italia Agosti 2014, lakini akashindwa kurejesha uwekezaji huo baada ya kucheza mechi 16 za Ligi Kuu, huku akifunga bao moja tu.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU