Malaika atoboa siri ya mastaa kubwia unga

Malaika atoboa siri ya mastaa kubwia unga

607
0
KUSHIRIKI
Malaika Exavery

NA JOHANES RESPICHIUS,

NYOTA wa muziki wa Bongo Fleva, Malaika Exavery, amesema ongezeko la wasanii kutumia dawa za kulevya linachangiwa na matumizi mabaya ya fedha na kutokujiandaa kiakili wakati wakivuma.

Malaika ameliambia Papaso la Burudani kuwa, umaarufu ni kitu cha kupita, hivyo wasanii hujikuta wamepitwa na wakati ilhali hawajawekeza popote.

“Sababu kubwa inayofanya wasanii watumie dawa za kulevya ni msongo wa mawazo. Msanii anapojikuta hana kitu chochote cha kuendesha maisha yake na aliwahi kuwa maarufu huona njia nyepesi ya kuondoa msongo wa mawazo ni kutumia dawa za kulevya,” alisema Malaika, msanii anayefanya vyema na wimbo unaoitwa Rarua.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU