Schweinsteiger agoma kuondoka Man Utd

Schweinsteiger agoma kuondoka Man Utd

526
0
KUSHIRIKI
Bastian Schweinsteiger

LONDON, England

TIMU ya Manchester United imesema kuwa ipo tayari kuchukua pauni milioni 14 ili imuachie kiungo wake, Bastian Schweinsteiger, lakini inavyosemekana staa huyo amegoma kuitema klabu hiyo.

Kiungo huyo wa timu ya Taifa ya Ujerumani amekuwa na kipindi kigumu tangu alipojiunga na klabu hiyo ya Old Trafford na inasemekana hatima yake ipo shakani baada ya kukumbwa na majeraha.

Man United kwa sasa inasemekna kuwa inatafuta njia ya kumtema nyota huyo, lakini italazimika kumlipa fedha zilizobaki katika mkataba wake wa miaka miwili.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU