Shilole akanusha kutoka kimapenzi na Gaucho

Shilole akanusha kutoka kimapenzi na Gaucho

707
0
KUSHIRIKI
Zuwena Mohamed ‘Shilole’

Na JOHANES RESPICHIUS,

BAADA ya kuenea kwa taarifa kuwa msanii Zuwena Mohamed ‘Shilole’ anatoka kimapenzi na msanii anayemsimamia kimuziki kupitia lebo yake ya Shilole Entertainment, Gaucho, mkali huyo  amekana tuhuma hizo.

Shilole ameliambia Papaso la Burudani kuwa lengo la kuanzisha lebo hiyo ni kuwasimamia wasanii wachanga kimuziki na siyo kutoka nao kimapenzi, hivyo taarifa hizo siyo za kweli.

“Lebo yangu inajihusisha na muziki pekee na siyo mambo ya mapenzi, Gaucho ana mpenzi wake na mimi pia nipo kwenye uhusiano na mpenzi wangu, kwa hiyo hizo siyo taarifa za ukweli kabisa,” alisema Shilole.

Aliongeza kuwa baada ya Gaucho kufanya vizuri, mashabiki watarajie kumsikia msanii mwingine mpya wa kike kutoka kwenye lebo yake.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU