Muhogo Mchungu akosoa uandaaji wa filamu

Muhogo Mchungu akosoa uandaaji wa filamu

690
0
KUSHIRIKI
Muhogo Mchungu

NA GLORY MLAY,

MKONGWE wa maigizo nchini, Abdallah Mkumbila ‘Muhogo Mchungu’, amesema maandalizi kabla ya wasanii kuanza kufanya filamu ni muhimu kwani huchangia kuongeza ubora wa kazi.

Muhogo Mchungu, ameliambia Papaso la Burudani kuwa msanii kabla hajaingia lokesheni inatakiwa awe amefanyiwa maandalizi ya kisaikolojia na mwonekano ili aweze kuuvaa uhusika.

“Ili msanii aweze kufanya kile kilichoandikwa kwenye mwongozo yaani script, ni lazima awe tayari amejiandaa au kuandaliwa kisaikolojia si tu kufanyiwa make up, hilo ni muhimu ila kwenye filamu zetu nyingi kitu hicho hakifanyiki,” alisema Muhogo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU