Samoura: UN imenijenga kuwa kiongozi

Samoura: UN imenijenga kuwa kiongozi

315
0
KUSHIRIKI
Fatma Samoura

LONDON, England

KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni (Fifa), Fatma Samoura, amesema kufanya kazi kwa muda mrefu ndani ya Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kulimkomaza kikazi kabla ya kupewa kibarua cha ukatibu mkuu wa shirikisho lenye mamlaka ya soka.

Alisema hayo alipokuwa akizungumza na Shirika la Habari England, BBC, ambapo aligusia maeneo yenye migogoro alikofanyia kazi zake za kisiasa na vita kama Afghanistan, Liberia, Sierra Leone, Timor Mashariki, Kosovo na Nigeria.

“Nafikiri kwa zaidi ya miaka 20 UN nilikuwa najiandaa kwa ajili ya hii kazi,” alisema.

Samoura,  ambaye ni katibu mkuu wa kwanza mwanamke katika historia ya shirikisho hilo la mpira wa miguu ulimwenguni, alichukua nafasi ya aliyekuwa katibu mkuu, Jerome Valcke, ambaye alifungiwa kujihusisha na masuala ya soka kwa miaka 12, baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika na rushwa michezoni.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU