Chelsea, Liverpool, Juventus zamwania kinda FC Porto

Chelsea, Liverpool, Juventus zamwania kinda FC Porto

302
0
KUSHIRIKI
Ruben Neves

LONDON, England

TIMU za Chelsea, Liverpool na Juventus zinasemekana kuwa kwenye vita kali zikimwania kinda wa FC Porto mwenye umri wa miaka 19, Ruben Neves, ili kuona kama zitaweza kupata huduma yake kuanzia majira ya baridi yajayo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Visao de Mercado, makachero wa vigogo hao wa soka England na Italia wamekuwa wakipigana vikumbo katika ofisi ya klabu hiyo ya Ureno ili kuona nani atakuwa wa kwanza kunasa saini ya kinda huyo mwenye thamani ya pauni milioni 18.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU