Oxlade-Chamberlain naye awazia kuitema Arsenal

Oxlade-Chamberlain naye awazia kuitema Arsenal

508
0
KUSHIRIKI

LONDON, England

KIUNGO wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain, amesema kuwa anatafakari kuitema klabu hiyo endapo kocha wake,  Arsene Wenger ataendelea kumweka benchi.

Hatua hiyo imekuja baada ya Oxlade-Chamberlain kucheza mechi tatu kwenye kikosi cha kwanza tangu msimu huu wa ligi kuu uanze.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 23, alijiunga na Gunners mwaka 2011 lakini hadi sasa ameshafunga mabao nane katika kipindi cha miaka mitano aliyoitumikia klabu hiyo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU