Vigogo AC Milan wamtaka Lamela

Vigogo AC Milan wamtaka Lamela

546
0
KUSHIRIKI
Erik Lamela

MILAN, Italia

TAARIFA kutoka nchini Italia zinaeleza kuwa vigogo wa timu ya AC Milan wapo katika mchakato wa kumsajili winga wa Tottenham, Erik Lamela wakati wa usajili wa majira ya baridi yajayo.

Kwa mujibu wa jarida la Calciomercato.

Mkurugenzi Mkuu Mtendaji  wa AC Milan, Marco Fassone na Mkurugenzi wa Michezo, Massimo Mirabelli, wiki iliyopita wanaripotiwa kuwa jijini London kwa ajili ya kuanza mazungumzo na Spurs kuona kama watamsajili staa huyo wa timu ya Taifa Argentina.

Lamela alisajiliwa na Tottenham akitokea kwa vigogo wengine kwenye michuano hiyo ya Serie A, AS Roma miaka mitatu iliyopita.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU