Adhabu ya Mourinho yamkutanisha na Wenger

Adhabu ya Mourinho yamkutanisha na Wenger

869
0
KUSHIRIKI

Manchester, England

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho, amefungiwa kukaa benchi mechi moja na kupigwa fainali ya pauni 50,000 na Chama cha Soka cha England (FA).

Adhabu hiyo itamfanya kuikosa mechi dhidi ya Swansea, lakini atarejea dimbani kukumbana na hasimu wake, Arsene Wenger, kwenye mchezo wa Ligi Kuu England, Novemba 19 mwaka huu.

Mourinho anadaiwa kukubali kosa la kumzungumzia mwamuzi Anthony Taylor, wakati wakikaribia kukutana na Liverpool mwezi uliopita waliotoka sare ya 0-0, lakini alikataa kuharibu mchezo huo kwa maneno yake.

Kamati ya maadili imemkuta na kosa hilo, hivyo pamoja na adhabu hiyo na kupigwa faini, Mourinho ataangaliwa mwenendo wake siku za usoni.

Pamoja na kosa kutoa maelezo kuhusiana na mwamuzi Taylor, pia adhabu hiyo imeambatana na kosa la kocha huyo kumfokea mwamuzi Mark Clattenburg, aliyekataa kutoa penalti baada ya mchezaji wake, Matteo Darmian, kuangushwa na Jon Flanagan.

Tukio hilo lilitokea kwenye mchezo dhidi ya Burnley uliomalizika kwa sare Jumamosi ya wiki iliyopita.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU