YANGA YAIRAHISISHIA KAZI SIMBA

YANGA YAIRAHISISHIA KAZI SIMBA

2740
0
KUSHIRIKI

NA ZAITUNI KIBWANA

SIKU chache baada ya Yanga kusema kuwa hawana nafasi ya kumsajili kiungo wa Simba, Jonas Mkude, kazi imekuwa rahisi kwa Simba, baada ya nahodha huyo kuapa kutoondoka kwenye kikosi hicho.

Mkude, mwenye uwezo wa kumiliki mpira na kufanya kazi ya kuwalinda mabeki wake, huku pia akifanya kazi ya kupanga mashambulizi, mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu.

Akizungumza na BINGWA, Mkude alimewatoa wasiwasi mashabiki wa Simba na kusema kuwa, hawezi kwenda popote pale zaidi ya kubaki kwenye kikosi hicho cha Msimbazi.

“Siwezi kuondoka Simba, mashabiki wala wasiwe na wasiwasi, kwani siendi popote pale zaidi ya kubaki Msimbazi,” alisema.

Mkude, ambaye huwa anatumika kama sentahafu wakati mwingine kwenye kikosi hicho cha Joseph Omog, alisema kuwa tayari ameanza mazungumzo na mabosi wake wa Simba ili kuongeza mkataba mpya.

“Nimeanza mazungumzo, ikiwemo kurekebishiwa baadhi ya vipengele kwenye mkataba wangu hivyo nina imani hatuwezi kushindwana na nitasaini mkataba tu.

“Nitasaini tu, ila kwa makubaliano ambayo tutakubaliana sina shaka kabisa na hilo,” alisema.

Mkude na nyota wengine kama kiungo Said Ndemla na straika Ibrahim Ajib, watamaliza mikataba kati ya Desemba, mwaka huu na Juni, mwakani.

Ukiacha nyota hao, nyota wengine ambao wako mwaka wa mwisho wa mikataba yao ni kipa Vincent Angban, beki Jjuuko Murushid na kiungo Mwinyi Kazimoto.

Simba, ambao ndio vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, tayari imeanza kufanya mazungumzo na nyota hao kwa ajili ya kuwaongezea mkataba mipya.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU