EZEQUIEL LAVEZZI; MURGENTINA ANAYEWAKIMBIZA RONALDO, MESSI KATIKA MSHAHARA

EZEQUIEL LAVEZZI; MURGENTINA ANAYEWAKIMBIZA RONALDO, MESSI KATIKA MSHAHARA

456
0
KUSHIRIKI
during the pre-season friendly match between SSC Napoli and Paris Saint-Germain FC at Stadio San Paolo on August 11, 2014 in Naples, Italy.

LONDON, England

HUENDA mpaka sasa ulimwengu wa soka haujashuhudia wanasoka wenye vipaji vya hali ya juu kama walivyonavyo mastaa Lionel Messi na hasimu wake, Cristiano Ronaldo.

Kutokana na hilo, kuna uhakika mkubwa kuwa mashabiki wengi wa soka wanaamini wawili hao ndio wachezaji wanaolipwa vizuri zaidi kwenye ulimwengu wa soka.

Ni kweli Ronaldo, anayekipiga Real Madrid na Muargentina Messi wa Barcelona wanapokea mpunga wa kufa mtu, lakini hilo haliwafanyi kuongoza orodha ya wanasoka wanaovuna fedha nyingi kila mwishoni mwa wiki.

Hivi karibuni, Ronaldo akiwa sambamba na staa mwenzake wa Madrid, Gareth Bale, walisaini mikataba minono ya kuendelea kukipiga Bernabeu.

Ronaldo, ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa ya Ureno, alisaini mkataba ambao utamfanya kuweka mfukoni kitita cha Dola za Marekani 743,000 kwa wiki.

Hata hivyo, kiasi hicho cha fedha ni kidogo mno kumfanya kuwa kinara wa wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa duniani.

Kwa upande wake, Messi, ambaye wiki chache zilizopita alikuwa kwenye wingu zito na mabosi wake, Barca baada ya kugoma kumwaga wino, alisaini mkataba mpya ambao utamfanya kuingiza Dola 456,000 kwa wiki. Lakini pia ni mshahara mdogo na hawezi kuongoza kwenye orodha ya wachezaji wanapokea mshahara mkubwa kila mwishoni mwa wiki.

Kwa maana nyingine, achana na mastaa hao wanaoaminika kuwa ndio wenye ubora wa hali ya juu wanapokuwa uwanjani.

Kwa mujibu wa taarifa zilizovujishwa na mtandao wa Football Leaks, wachezaji hao wote hawamfikii Ezequiel Lavezzi, anayekipiga Ligi Kuu nchini China.

Muargentina huyo ndiye nyota anayepokea mshahara mkubwa kuliko wote na si tu barani Ulaya, bali hata duniani kote.

Imeelezwa kuwa, Lavezzi, ambaye anakipiga na Messi katika kikosi cha timu ya Taifa ya Argentina, analipwa mara mbili ya mshahara anaopokea Messi, ambaye ni mshindi mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or.

Alijiweka katika ramani hiyo ya wanasoka wanaopokea fedha nyingi tangu alipohama Ulaya na kujiunga na moja ya klabu kubwa kule China.

Lavezzi, mwenye umri wa miaka 31, alitua Hebei China Fortune Februari mwaka huu akitokea Paris Saint-Germain, ambako alikuwa akikinga Dola 7,626,667 kwa wiki.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, kiungo huyo alisaini mkataba unaomfanya kukinga pauni 400,000 kwa wiki na kiasi hicho cha fedha kinamfanya kuwafunika Ronaldo na Messi.

Taarifa nyingine zimedai kuwa, huenda nyota huyo anapokea zaidi ya kiasi hicho cha fedha ambacho ni baada ya makato ya kodi.

Kwa mpunga huo wa wiki, staa huyo amemzidi Messi kwa Dola 370,000.

Licha ya kupokea fedha hizo nyingi, Lavezzi, ambaye alikuwa akikipiga Napoli, hajafanikiwa kupachika hata bao moja tangu alipotua China.

Msimu uliopita, mkali huyo alicheza mechi 10 za ligi kuu, lakini hakuweza kupasia nyavu. Kwa upande mwingine, Lavezzi hawezi kumzidi Ronaldo linapokuja suala la utajiri wa jumla.

Ambacho Lavezzi amemzidi Ronaldo ni mshahara tu na si mapato mengine, yakiwemo yale yanayotokana na mikataba ya matangazo.

Juni mwaka huu, Ronaldo alikuwa kinara wa wanasoka wenye kipato kikubwa duniani.

Taarifa iliyotolewa na Jarida la Forbes lilimtaja staa huyo wa zamani wa Manchester kuwa ndiye mchezaji mwenye kipato kikubwa akiwa na utajiri wa Dola za Marekani milioni 88.

Jarida hilo maarufu nchini Marekani, liliweka wazi kuwa mwanasoka huyo anaingiza Dola milioni 56 kutokana na bonsai, huku mikataba yake ya matangazo ikimuingizia Dola milioni 32.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU