UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU [63]

643
0
KUSHIRIKI

Ilipoishia jana

RAMONA

Ndege ya shirika la Qatar Airways ilikuwa inatua Uwanja wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, jijini Dar es Salaam nchini Tanzania. Ramona alishuka akiwa pamoja na walinzi wake watano. Alikuwa na moyo ule ule moyo wa ajabu uliotaka kwenda kumwambia mama yake na Roika juu ya kilichompata mwanaye na kumwomba msamaha.

SASA ENDELEA

Ramona hakujali kuwa mama yake na Roika ataweza kumshtaki pindi atakapojua kuwa yeye amemuua mtoto wake. Hata kama alikuwa ana uwezo wa kukimbia, lakini hakupanga kufanya hivyo. Hakupanga kukwepa lolote, hata kama mama yake Roika ataviita vyombo vya dola.

Mateso aliyokuwa anayapata juu ya kifo cha Roika, ndiyo yaliyomfanya kuchukua uamuzi huo mgumu. Ingawa alijua kuwa uamuzi huo atamuumiza mama wa watu, lakini aliona kufanya hivyo ni busara zaidi, kwani alijua mama yake Roika, hatakuwa akifahamu jambo lolote lililompata mwanaye nchini Pakistani.

Siku za nyuma, Roika alishawahi kumwelekeza Ramona nyumbani kwa mama yake, mahali alipozaliwa na kukulia. Japo Ramona hakuwahi kufika, lakini maelekezo aliyowahi kuyapata toka kwa Roika, aliamini kuwa yanaweza kumfikisha.

Baada ya kutoka Uwanja wa Julius Kambarage Nyerere, Ramona akiwa na walinzi wake watano, waliingia kwenye magari mawili yaliyokuwa yametayarishwa kwa ajili yao.

ISLAMABAD

Tayari ndege ilikuwa imetulia uwanja wa Islamabad nchini Pakistani, kwa muda huo ilikuwa ni saa 3:30 usiku. Roika alishuka haraka ndani ya ndege bila kufuata foleni ya abiria wenzake. Aliiangalia saa yake ya mkononi iliyozidi kumpa wasiwasi mkubwa na hofu ya moyo, kwani kichwa chake kwa muda wote kilikuwa kikimuwaza mwanamke ambaye, tayari ndani ya moyo wake, alikuwa amekwishafunga naye ndoa. Jina la Shazayi kwake lilikuwa ni jina la thamani. Alijikuta anampenda mwanamke huyo kupita kiasi cha kupenda.

Katika zile siku tatu ambazo daktari alikuwa amemwambia Roika kuwa, Shazayi atakuwa mzima, hazikubaki tena siku. Bali yalibaki masaa. Masaa manne yalibaki kwa  Shazayi kuwepo kwenye uso wa dunia. Hivyo Roika alikuwa na muda mchache wa kuwahi hospitalini kabla mshale wa saa haujafika kwenye namba sita.

Kama mtu aliyechanganyikiwa, aliingia kwenye taksi haraka na kumwambia dereva ampeleke hospitali ya Mohamed Words. Hospitali ya Mohamed Words ilikuwa kaskazini mwa jiji la Islamabad umbali unaogharimu saa moja na dakika 45.

“Mr unaonekana unaharaka sana je unataka kufika huko kabla ya saa ngapi?” dereva taksi aliuliza.

“Kabla ya saa tano naomba tuwe tumefika tafadhari,” alijibu Roika.

“Mimi naweza kukufikisha muda uutakao, lakini kikwazo cha kuchelewa kitakuwa ni polisi,” aliongea dereva.

“Kwa nini unasema polisi ni kikwazo?”

“Mitaa yote na miji yote, polisi wamezagaa kwenye vizuizi na kwenye vituo mbalimbali, wakikagua kila gari linalopita kwenye barabara za Pakistani.”

“Kwa nini?”

“Kwa sababu mtoto wa Rais amepotea katika mazingira ya kutatanisha, hivyo serikali na vyombo vyake vyote vya dola viko katika zoezi la kumtafuta. Umakini huo wa serikali umeanza tokea leo asubuhi.”

Roika aliposikia hivyo, alizidi kuchanganyikiwa, hakika alipoteza mwelekeo wa mawazo yake. Kwani hakufahamu  kuwa tayari serikali ilikuwa imekwisha jua kuwa Shazayi mtoto wa Rais hajulikani mahali alipo. Ndio kwanza alikuwa anasikia kutoka kwa dereva taksi.

Mwanzoni Roika alikuwa akihofia kutofika hospitalini kwa wakati au kufika na kukuta tayari Shazayi amekwisha kufa, lakini kwa muda huo, hofu nyingine ilikuwa imeingia, hofu ya kukamatwa na vyombo vya dola endapo serikali itakuwa inajua kitu kuhusu yeye. Hakika alichoka na kuwaza mambo mengi yaliozidi utawala wake wa kichwa.

Tayari dereva alikuwa amekwisha washa gari na kuwa mbali na uwanja wa ndege. Roika alimwambia dereva.

“Tumia akili zako zote ili tufike hospitalini kabla ya hiyo saa tano, nami natumia akili zangu zote kuwajibu askari maswali kwa haraka, pindi watakapo tusimamisha. Kama tutawahi kufika nitakupa dola 300 ( shilingi laki tano)”

Pesa alizomuahidi dereva zilikuwa ni nyingi, kwani bei halisi ya kutoka uwanja wa ndege hadi mji wa Alamayana kunako hospitali ya Mohamed Words ni dola 80. Hivyo dereva alikaa sawa na kuweka nia kwenye usukani, kwani fedha hizo zingeweza kumfanya alihegeshe gari nyumbani kwake kwa siku mbili, ashinde anapumzika.

MOHAMED WORDS

Yeye kama daktari, sasa aliamini kuwa Shazayi anakwenda kufariki dunia, dakika chache zijazo. Alitamani  kumpigia simu Roika, amuulize kwa muda huo yuko wapi, amuulize kama alifanikiwa kuipata damu au la, lakini hakuwa na namba yake ya simu. Kwani Roika alipokuwa anaondoka pale hospitalini hakubeba kitu chochote. Muda mwingine aliamini kuwa huenda Roika amekwisha fia njiani, kwani pindi alipokuwa anaondoka pale hospitali ile juzi,  hali yake ilikuwa mbaya.

Roho yake ilikuwa ikimuuma, pindi alipoutazama uzuri wa Shazayi huku wasiwasi na hofu vikizidi zaidi wakati alipokuwa akisikia sauti za ving’ola nje ya hospitali, ving’ola vya magari ya polisi, magari yaliokuwa yakizunguka mji mzima wa Alamayana. Ikionyesha kuwa polisi hao walikuwa wakihenya kila mahali kumtafuta mtoto wa Rais.

Nini kitafuatia, usikose Jumatatu.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU