RAY C AINGILIA KATI BIFU LA ALI KIBA, DIAMOND

RAY C AINGILIA KATI BIFU LA ALI KIBA, DIAMOND

2041
0
KUSHIRIKI

NA ZAITUNI KIBWANA,

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Rahema Chalamila ‘Ray C’, ameingilia kati bifu la wasanii wenzake Ali Kiba na Naseeb Abdul ‘Diamond’, kwa kuwataka wawili hao sasa kushirikiana.

Ray C alitoa kauli hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram pale alipohoji nini maana ya bifu na zina haja gani kwa maendeleo ya muziki?

Mwanadada huyo aliyetamba na nyimbo mbalimbali kama Nataka Niwe na Wewe Milele aliendelea kwa kusema kuwa muda ufike kwa wasanii kupendana.

“Muziki ni hisia, unaleta amani ya moyo, muda ufike wa sisi wasanii kupendana, kujaliana, kushirikiana kwani kazi yetu ni ile ile moja kuburudisha kama marubani wawili waendeshao ndege moja, lengo lao ni moja siku zote. Hebu fikiria umepanda ndege mara unaona marubani ghafla wamechenjiana wanapigana, kutakalika humo ndani kweli si utatamani utokee dirishani, ujue hapo hakuna kutua utasali sala zote usiombe. Hebu tupendane.”

Kauli hiyo ya Ray C iliwaibua mashabiki wake ambao waliwataja Ali Kiba na Diamond ambao wamekuwa kwenye bifu la muda mrefu ambalo linawagawa mashabiki wao.

Licha ya wawili hao kutotaja kisa cha mgomvi wao mpaka leo, juhudi mbalimbali zimefanyika kuwapatanisha ila zimeonekana kugonga mwamba baada ya wawili hao kuendelea kutopatana.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU