SHAMSA FORD: VIPODOZI ASILIA VINASAIDIA KUJENGA NDOA YANGU

SHAMSA FORD: VIPODOZI ASILIA VINASAIDIA KUJENGA NDOA YANGU

595
0
KUSHIRIKI

NA BEATRICE KAIZA

MSANII wa filamu za Bongo, Shamsa Ford, amesema licha ya kwamba ameolewa na kuzaa bado urembo wake hauwezi kupotea kwa kuwa anatumia vipodozi visivyo na kemikali ambavyo pia kwa kiasi kikubwa vinachangia kuimarisha ndoa yake.

Nguli huyo katika filamu nchini amesema kuwa yeye ni tofauti na wasanii wengine wa kike wenye mawazo finyu ya kusema kwamba kitendo cha wao kuzaa kitawapotezea mvuto waliokuwa nao kabla ya kupata mtoto au watoto.

Akizungumza na BINGWA, Ford ambaye aliolewa hivi karibuni alisema kwamba vipo vitu anavyoamini vinamfanya mwanamke aendelee kuonekana mrembo licha ya kuzaa na kusema kuwa watu wanaodanganyana kuwa kuolewa na kuzaa kunapoteza urembo wanapotoshana.

Diva huyo anasema mwanamke au msichana kufunga ndoa na kuzaa si chanzo cha kukaa mbali na masuala ya urembo kwani bado anatakiwa kuwa na mvuto zaidi ili kuijenga ndoa yake.

“Mara nyingi nimesikia watu wakisema kuwa mtu akifunga ndoa au kujifungua yeye na mambo ya urembo basi! Mfano mimi nimeolewa na nina mtoto lakini bado siwezi kuacha kupendeza na kuwa msafi,” anasema.

Anasema kitu cha muhimu zaidi kinachomsaidia kubaki na urembo wake ni kufanya mazoezi na kutumia vitu vya asili kwenye mwili wake.

“Asikudanganye mtu, hata kama hujazaa mwanamke lazima uzingatie masharti ya urembo na kufanya mazoezi mara kwa mara, kwa sababu mwili ukizoea mazoezi mvuto haupotei kamwe.

“Kingine niwaase wakinamama wapunguze kutumia vipodozi vyenye kemikali, mimi uso wangu huwa naupendezesha kwa vipodozi vya asili kama mayai ya kienyeji na manjano ili kuifanya ngozi yangu iwe imara zaidi.

Aidha, Ford alitoa neno kwa wanawake akiwataka wajipende ili wawe na ndoa imara, akimaanisha kuwa kujiheshimu kwa mwanamke ndio ‘uchawi’ wa kuifanya ndoa idumu.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU