ALAN RUSCHEL AMTAJA ALIYENUSURU MAISHA YAKE KWENYE AJALI YA CHAPECOENSE

ALAN RUSCHEL AMTAJA ALIYENUSURU MAISHA YAKE KWENYE AJALI YA CHAPECOENSE

682
0
KUSHIRIKI
Alan Ruschel

CHAPECO, Brazil

MMOJA wa wachezaji walionusurika kifo katika ajali ya ndege iliyoihusisha timu ya soka ya Chapecoense, Alan Ruschel, ameibuka na kumtaja aliyenusuru maisha yake kwenye ajali hiyo ya kusikitisha iliyotokea Novemba 28 mwaka huu.

Timu hiyo ya Brazil ilikuwa safarini kuelekea nchini Colombia kabla ya ndege waliyoipanda kudondoka na kuua watu 71 huku wengine sita tu wakinusurika.

Kwa mara ya kwanza, Ruschel alionekana hadharani wiki iliyopita katika mchezo maalumu wa hisani kwa Chapecoense, ambapo alinukuliwa akisema kuwa bila ya Jackson Follman asingeendelea kupumua hadi sasa.

Follman pia alikuwa ni mmoja wa walionusurika kifo kwenye ajali hiyo lakini kwa bahati mbaya alipoteza mguu wake mmoja, kabla ya Chapecoense kumwahidi ajira ya kudumu ndani ya timu hiyo.

“Follman aliniita na kuniambia, ‘njoo ukae nami’ na niliitikia wito kwani ni mtu ninayemjua tangu 2007, hivyo nikainuka nilipokaa na kwenda kuketi karibu na yeye.

“Kumbe wito huo uliniokoa na kifo,” alisema.

“Safari ilikuwa nzuri tu kabla ya kushangazwa na taa za kawaida kuzimika ghafla na taa ya dharura ikawaka.

“Nikamuuliza Helio Neto (mchezaji mwingine aliyepona) kama amesikia kitu chochote, akajibu hapana na akaanza kusali, akimuomba Mungu atulinde sote. Na hapo sikumbuki kilichoendelea,” aliongeza.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU