VAN DIJK ATINGA JEZI YA MAN CITY

VAN DIJK ATINGA JEZI YA MAN CITY

550
0
KUSHIRIKI
Virgil van Dijk

LONDON, England

WAKATI timu nyingine zikiendelea kuifukuzia saini yake, beki mahiri wa kati wa Southampton, Virgil van Dijk, mapema wikiendi jana ameonekana akiwa na jezi ya Manchester City ambayo ni mojawapo ya timu hizo zinazomwania, patamu hapo.

Van Dijk ameibuka kuwa beki imara mno katika kipindi cha miezi michache ya hivi karibuni na miamba ya soka ya Ligi Kuu England imeanza kuifukuzia saini yake kabla ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa Januari mwakani.

Man City, Liverpool na Man United ndio timu tatu zinazoisaka saini yake, huku City ikiweka wazi ofa yao ya pauni milioni 50 kwa ajili yake.

Jezi hiyo ya City aliyoivaa ilitoka kwenye zawadi ya siri ya Krismasi na beki mwenzake, Jose Fonte ndiye aliyeivujisha picha hiyo kwenye ukurasa wa Instagram akiwa na wachezaji wengine wa Southampton.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU