UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

654
0
KUSHIRIKI

Ilipoishia Jumanne

MOYO wake ulimdunda zaidi ya ngoma, mwili wake ulitetemeka. Taratibu alianza kuusogeza uso wake kuelekea kwa Shazayi. Hakika ilikuwa ni siku ya muujiza. Shazayi alikuwa anamtazama Roika kwa tabasamu zuri ajabu. Macho yake mazuri mithili ya malaika mtoto, yalikuwa yakitokwa na machozi. Hakika Shazayi aliionekana ni mwanamke mzuri kama mtu aliyetokwa kuzaliwa upya.

SASA ENDELEA

Licha ya uchomvu mkubwa aliokuwa nao, Shazayi aliendelea kutabasamu, akimtazama Roika aliyekuwa akitokwa na machozi muda wote. Furaha kubwa ilikuwa imewatala kwa wote wawili.

Macho mazuri ya Shazayi binti wa Kiarabu, yalikuwa yakimtazama kijana wa Kiafrika Roika. Roika aliusogeza uso wake karibu na uso wa Shazayi, akambusu kwenye paji lake la uso, busu lililomtoa Shazayi machozi.

“Roika nakuona mume wangu,” aliongea Shazayi kwa furaha isiyoelezeka kwa urahisi.

“Hakika hata mimi nakuona mke wangu,” alijibu Roika kwa sauti nzuri na ya kubembeleza.

“Nilijua Mungu atakufanya uwe na nguvu ya kunikomboa nisipotee mbele yako na hakika umeweza.”

“Bila shaka Shazayi. Mungu alinifanya kusafiri mbali kwenda kutafuta msaada.”

“Roika tazama ninavyokupenda, tazama unavyonipenda ni nani atakayeweza kuikatisha safari yetu ya milele. Usiniache Roika, niko tayari kufa kwa ajili yako. Siipendi dunia, bali nakupenda wewe. Nilikuwa tayari kuwaachia wazazi wangu machozi ili wewe uutambue upendo wangu kwako. Nakupenda sana, tangu sasa mimi ni mali yako, nifanye vile upendavyo.”

“Shazayi maneno yako yataendelea kuishi. Upendo wangu kwako hauwezi kusimuliwa hata kwa kuandikwa kwenye vitabu vya maktaba nzima.”

“Nilipokuwa ndotoni, nilimuona malaika akituunganisha kuwa mwili mmoja. Wewe ukitokea Afrika nami nikitokea nchi hii ya Kiarabu. Amini nakwambia Roika, Allah ametutoa mbali tusifanye makosa na mkono wake. Nakupenda Roika.”

“Nakupenda Shazayi.”

Hakika yalikuwa ni maneno ya kupendeza pindi wawili hawa walipokuwa wakizieleza hisia zao.  Upendo wao ulionekana si wa kawaida. Kwao yalikuwa ni zaidi ya mapenzi.

Baada ya maongezi hayo, Roika alimuaga Shazayi kuwa anakwenda hotelini. Lakini Shazayi alimtaka awe makini kwa sababu kikundi cha Swaba kitakuwa bado kikimsaka kwa sababu, alimuokoa kabla ya kuchomwa moto.

“Shazayi nataka nikautoe wasiwasi uongozi wa hoteli, wasije kutoa taarifa  polisi, kwamba mimi nimepotea,” aliongea Roika.

“Sawa mpenzi, naomba uwahi kurudi kwani kuna hadithi nzuri nataka kukusimulia,” alijibu Shazayi.

“Usijali mpenzi,” alijibu Roika huku akimbusu Shazayi.

Baadaye Roika alitoka Hospitali ya Mohamed Words na kumuacha Shazayi. Aliingia kwenye taksi na kuondoka hospitalini hapo, akishika njia ya kuelekea mji wa Nuruwan kunako Hoteli ya Alashak.

Akiwa ndani ya taksi, Roika alimkumbuka Ramona.

“Sitaki ajue kuwa mimi ninaishi.  Naomba Mungu nikamilishe ndoa yangu na Shazayi haraka, kisha tuondoke kurudi Tanzania. Lakini namhofia baba yake, sijui kama mimi mtu mweusi nitafanikiwa kumuoa binti wa Kiarabu,” alijisemea Roika.

“Lakini nitatumia njia nzuri na ajabu itakayomfanya Rais Galim anipe binti yake kwa mikono yake miwili, akiwa ameridhia kwa moyo mmoja. Ramona utanisamehe siwezi kuishi na wewe. Upendo wangu kwako haupo tena, si kwa sababu ulinipiga risasi la hasha, bali kwa sababu mwanamke mwenzio aliye na nguvu kuzidi zako,  amekwisha nichukua.  Nami ni mali yake. Biyanah najua unanipenda, lakini wewe si mwanamke ambaye Mungu amenipa, hivyo tafuta sehemu mpya, kwani mimi napenda vitu ambavyo  Mungu amenichangulia,” Roika aliongea peke yake akiwa ndani ya taksi.

TANZANIA

Msamaha mkuu alikuwa umeupata Ramona kutoka kwa mama Roika. Hakuamini kabisa kusamehewa bado nafsi yake na akili yake vilitawaliwa na mashaka.

Baada ya Dina kuingia, alielekea kukaa kwenye kochi. Alipomtazama mama yake na mgeni, alipatwa na mashaka, hakuelewa nini kilikuwa kikiendelea pindi yeye alipokuwa amekwenda sokoni. Aliamua kukaa kimya.

“Dina nenda ukaanze kutayarisha chakula,” aliongea mama yake.

“Mama mbona unanitoa mara kwa mara hata mgeni sijamfahamu?” aliongea Dina akiwa amekasirika.

“Unataka kumfahamu mgeni tu?”

“Ndio mama nina haki hiyo. Kwa kuwa mimi pia ni mwenye nyumba.”

“Sawa, nitakwambia nenda kwanza ukabandike sufuria jikoni,” aliongea mama Roika huku akimgeukia Ramona.

Dina alinyanyuka haraka na kwenda jikoni.  Baada ya Dina kutoka mama Roika alimwambia Ramona.

“Mwanangu, usione namtoa binti yangu mara kwa mara. Nataka asijue kuwa kaka yake amekwisha kufa. Maana akijua naweza kumpoteza. Kwani anaugonjwa wa mshtuko, pindi anaposikia habari mbaya. Mara ya kwanza aliwahi kuanguka pindi baba yake alipofariki. Mara ya pili alianguka pindi aliposhika utatu darasani, kwa sababu alikuwa anashika ukwanza siku zote. Hivyo nitamficha siri hii hadi pale nitakapopata muda mwafaka wa kumwambia.”

Ramona aliposikia hivyo, alianza kulia tena, maana maneno hayo yalizidi kumuumiza yeye kama muuji wa mmoja wa familia ile.”

“Usilie mwanamngu, tayari tumekwisha sameheana. Ninachotaka tu binti yangu asijue lililompata kaka yake.”

“Mama najiona ni mwenye dhambi. Naumia pindi napowatazama wewe na huyu mwanao. Kwa kuwa mimi ni chanzo cha nyie kuishi bila Roika,” aliongea Ramona.

Nini kitafuatia usikose kesho

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU