BRADLEY: JAMANI SWANSEA MMENIONEA

BRADLEY: JAMANI SWANSEA MMENIONEA

384
0
KUSHIRIKI
Bob Bradley

CARDIFF, Wales

BAADA ya kufungashiwa virago na klabu ya Swansea, Kocha Bob Bradley amesema alitamani kuiona timu hiyo ikimuamini na kumpa muda wa kuweka mambo sawa na kuendelea kuinoa.

Kocha huyo alitimuliwa mapema wiki hii, baada ya mabosi wa Swansea kutoridhishwa na matokeo ya timu yao hiyo kwenye michezo 11 ambayo Bradley aliitumikia Swansea.

“Sidhani kama ulikuwa uamuzi sahihi, niliamini katika kazi yangu na nilishatambua kwamba nyakati zilikuwa ngumu.

“Klabu inatakiwa kujua kwamba kazi ilikuwa inakwenda vizuri, japokuwa matokeo tuliyoyataka hatukuyapata, hakuna kitu kigumu ukiwa kocha kama kugeuza matokeo ya timu ambayo inahaha kwenye janga la kushuka daraja.

“Natumai nitapata fursa ya kupata changamoto (kazi) nyingine,” alilalama Bradley.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU