DEPAY AFUMWA AKIVUTA SHISHA

DEPAY AFUMWA AKIVUTA SHISHA

435
0
KUSHIRIKI
Memphis Depay

ROTTERDAM, Uholanzi

WINGA asiye na maisha marefu ndani ya klabu ya Manchester United, Memphis Depay, amezidi kujipalia makaa ya moto baada ya kuonekana akivuta shisha wakati wa mapumziko yake nchini Uholanzi alikozaliwa.

Depay tangu atue United ameshindwa kupata namba ya kudumu ndani ya dimba la Old Trafford, baada ya msimu huu kuondolewa kwenye mipango ya kocha, Jose Mourinho.

Na tukio hilo la kukutwa akivuta kilevi hicho jijini Rotterdam sambamba na marafiki kadhaa wa kike, linategemewa kulegeza kuti lake alilokalia kwa sasa.

Depay alipigwa picha bila kujijua wakati akijiburudisha katika kiwanja cha bata cha Shisha and Tapas Lounge kilicho karibu na makazi yake saa 12 jioni na winga huyo anaendeleza orodha ya wanasoka waliowahi kubambwa wakitumia kilevi hicho kama vile Raheem Sterling, Gabriel Agbonlahor na Jack Wilshere.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU