GABRIEL KUAGWA KWA BATA NA MARAFIKI ZAKE

GABRIEL KUAGWA KWA BATA NA MARAFIKI ZAKE

627
0
KUSHIRIKI
Gabriel Jesus

SAO PAULO, Brazil

MSHAMBULIAJI kinda aliyesajiliwa na klabu ya Man City, Gabriel Jesus, anatarajiwa kuagwa kwa sherehe na mamia ya marafiki zake nchini Brazil wikiendi hii kabla ya kukwea pipa kuelekea jijini Manchester kuungana na wenzake.

Jesus aliyesajiliwa kwa dau la pauni milioni 27 kutoka Palmeiras, anatarajiwa kusafiri na ndege hadi England Jumatatu ya wiki ijayo akisubiriwa kukabidhiwa jezi namba 33 ndani ya dimba la Etihad.

‘Bata’ hilo linatarajiwa kufanyika jijini Sao Paulo mchana wa Jumapili na takribani wageni 500 wanatarajiwa kujumuika na kumtakia heri kinda huyo wa miaka 19 maisha mazuri ya Ligi Kuu England.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU