KIWANGO CHA ROJO, JONES CHAMKOSHA MOURINHO, APOTEZEA DILI LA LINDELOF

KIWANGO CHA ROJO, JONES CHAMKOSHA MOURINHO, APOTEZEA DILI LA LINDELOF

445
0
KUSHIRIKI

MANCHESTER, England

KLABU ya Manchester United chini ya Kocha Jose Mourinho, imeamua kupotezea mpango wake wa kumsajili beki wa kati wa Benfica, Victor Lindelof, mwenye thamani ya pauni milioni 38, baada ya kuridhishwa na viwango vya mabeki wake, Marcos Rojo na Phil Jones.

Tetesi zilianza kutesa kwenye vyombo vya habari kuwa, Lindelof huenda akatua United, huku mshambuliaji wa klabu hiyo, Zlatan Ibrahimovic, akichochea kuwa ni kijana mwenye uwezo wa kuchezea timu yoyote kubwa duniani.

Aidha, wakala maarufu, Jorge Mendes, pia alitajwa kuhusishwa katikati ya dili hilo ambapo wiki iliyopita iliripotiwa kwamba Mreno huyo alikwea pipa kuifuata Benfica kwa ajili ya mazungumzo na mchezaji huyo.

Ingawa vyombo vya habari vya Ureno vilidai kuwa dili lipo mbioni kukamilika, dili hilo limepigwa chini baada ya Mourinho kuridhishwa na machaguo ya walinzi wa kati aliyonayo kwa ajili ya mechi zilizobakia msimu huu.

Zaidi ya kuwa na machaguo ya kutosha, Mourinho kwa sasa anafurahia ‘kombinesheni’ nzuri kati ya Phil Jones na Marcos Rojo, waliorithi nafasi za Chris Smalling na Eric Bailly, ambao wanasumbuliwa na majeraha.

Hata hivyo, Bailly atakwea pipa kuungana na timu yake ya taifa ya Ivory Coast itakayoshiriki michuano ya Afcon Januari mwakani, lakini Mourinho ataendelea kupata ujeuri wa kutomsajili Lindelof kutokana na uwepo wa kitasa kingine cha Kiholanzi, Daley Blind.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU