KUMBE MIWANI ILIMHARIBIA BENTEKE LIVERPOOL

KUMBE MIWANI ILIMHARIBIA BENTEKE LIVERPOOL

740
0
KUSHIRIKI
Christian Benteke

MERSEYSIDE, Liverpool

WAKATI mshambuliaji Christian Benteke alipoondoka Liverpool, wengi wao walijua hahitajiki tena na kocha Jurgen Klopp, lakini hawakujua sababu ya kwanini hahitajiki.

Benteke alisajiliwa Liverpool na kocha wa zamani wa klabu hiyo, Brendan Rodgers, kutoka Aston Villa kwa dau la pauni milioni 32.5 mwaka 2015, lakini baada ya kocha huyo kutimuliwa na mikoba yake kupewa Klopp, Benteke alijikuta akipata wakati mgumu wa kumshawishi Klopp kiuchezaji.

Katika mahojiano aliyofanyiwa Klopp na gazeti la Liverpool Echo, kocha huyo alitania kwa kusema kuwa kitendo cha mshambuliaji huyo kuivunja miwani yake walipokuwa wanashangilia ushindi mtamu wa mabao 5-4 ndicho kilichofanya amuuze.

“Iliharibika kabisa na aliyeivunja alikuwa ni Benteke. Hivyo nitoe onyo kwa wengine, yeyote atakayevunja miwani yangu ya sasa atauzwa tu!” alichimba mkwara Klopp.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU