MSONGO WA MAWAZO WAHATARISHA MAISHA YA BONDIA

MSONGO WA MAWAZO WAHATARISHA MAISHA YA BONDIA

349
0
KUSHIRIKI

LONDON, England

BINGWA wa zamani wa dunia katika masumbwi, Ricky Hatton, ameibuka na kusema kwamba mara kadhaa amekuwa akijaribu kujiua katika vita yake ya kupambana na msongo wa mawazo.

Hatton, aliyewahi kuzichapa na mabondia kama Floyd Mayweather Jr na Manny Pacquiao, alikiri kuwa alikumbwa na msongo huo wa mawazo baada ya kustaafu mchezo wa ngumi.

“Mara kadhaa nilijaribu kujiua mwenyewe. Nilipenda kwenda baa na kunywa pombe, nilivyokuwa nikirudi nilichukua kisu, nakaa mwenyewe gizani na kuanza kulia,” alisema.

“Kulikuwa na nyakati ambazo hata kama sijapata kinywaji siku nyingi bado ningeweza kurudi nyumbani na rundo la mawazo likanijia. Hali hiyo ilitokea hata nilipokunywa kilevi.

“Lakini mwisho wa siku niliwaza kwamba, naweza kunywa hadi kufariki kwani sikuwa sawa kabisa, nikaanza kutumia na dawa za kulevya,” aliongeza bingwa huyo wa zamani wa mikanda ya dunia ya WBA (Super), IBF na IBO.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU