NEYMAR: NITAHAMIA KLABU HII NIKIONDOKA BARCA

NEYMAR: NITAHAMIA KLABU HII NIKIONDOKA BARCA

928
0
KUSHIRIKI
Neymar

CATALONIA, Hispania

HAKUNA timu yoyote kubwa barani Ulaya itakayomkataa winga wa Barcelona, Neymar, iwapo atahitaji kuondoka kwa wakati huu, na Mbrazil huyo ameitaja timu ambayo angependa kuhamia atakapoamua kuikacha Barca.

Neymar alisema mara atakapoondoka Barca, atahamia katika timu ya Flamengo, ambayo ni wapinzani wa jadi wa timu yake ya zamani ya Santos ya nchini kwao, na lengo la kuhamia huko ni kucheza kwenye dimba la Maracana.

“Kama nikipata nafasi ya kuhama, ningependa kuhamia Flamengo, kwani nitajisikia faraja sana kucheza kwenye uwanja wa Maracana,” alisema Neymar, baada ya kucheza mchezo maalumu wa kuwakumbuka wahanga wa ajali ya Chapecoense.

Aidha, mchezaji mwingine mwenye mawazo ya kuungana na Neymar ni kiungo mwenzake, Rafinha, ambaye aliongeza: “Mungu akijaalia siku moja nitaichezea Flamengo.”

Lakini kwa wakati huu wawili hao watabaki Hispania kwa muda mrefu kwa ajili ya kukitumikia kikosi cha Kocha Luis Enrique.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU