TEVEZ KULIPWA MSHAHARA MNONO ZAIDI DUNIANI

TEVEZ KULIPWA MSHAHARA MNONO ZAIDI DUNIANI

804
0
KUSHIRIKI

SHANGHAI, China


MSHAMBULIAJI Carlos Tevez, ni rasmi sasa amekuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi duniani baada ya kujiunga na timu ya Shanghai Shenhua kwa dau la pauni milioni 77 kutoka Boca Juniors ya Argentina.

Aidha, Tevez ataipa faida timu yake hiyo kwa kitita cha pauni milioni 14 kitakachotoka kwenye ada ya uhamisho huo.

Tevez anajiandaa kuwa mchezaji atakayekuwa akilipwa pauni 615,000 kwa wiki ndani ya timu hiyo iliyopo jiji la Shanghai, ilipo timu aliyohamia kiungo wa zamani wa Chelsea, Oscar ya Shanghai SIPG.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU