AFCON 2017 MWANZO MWISHO

AFCON 2017 MWANZO MWISHO

806
0
KUSHIRIKI

LIBREVILLE, Gabon

FAINALI za Mataifa Afrika za mwaka huu Afcon 2017, itakuwa ni michuano ya 31tangu kuanzishwa kwake.

Awali mashindano ya mwaka huu yalipangwa kufanyika nchini Libya lakini ilishindikana na hali tete ya usalama nchini humo.

Mbio za kuwania taji la michuano hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) zitaanza kutimua vumbi Januari 14.

Jumla ya mataifa 16 yatatoana jasho kwenye mashindano hayo makubwa barani Afrika.

Timu hizo ni Gabon, Morocco, Algeria, Cameroon, Senegal, Misri, Ghana, Guinea-Bissau na Zimbabwe.

Nyingine ni Mali, Ivory Coast, Uganda, Burkina Faso, Tunisia, DR Congo na Togo.

Michezo ya hatua ya makundi itaanza kuchezwa Januari 14 hadi Januari 25.

Baada ya mapumziko mafupi, michezo ya hatua ya robo fainali itaanza kupigwa Januari 28 ambapo kinara wa kila kundi B atatoana jasho na mshindi wa pili kutoka Kundi A.

Mashabiki watakuwa tena uwanjani siku inayofuata, Januari 29, ambapo kinara wa Kundi C atavaana na mshindi wa pili wa Kundi D.

Hatua ya robo fainali itakamilishwa Januari 29 ambapo kinara wa Kundi D atakutana na mshindi wa pili wa Kundi C.

Michezo ya hatua ya nusu fainali itachezwa Februari mosi kabla ya mtanange wa kumsaka mshindi wa tatu kupigwa siku tatu baadaye (Februari 4).

Maashindano hayo yatafikia tamati Februari 5 kwa mchezo wa fainali.

——————————————————————-

Waamuzi wa Afcon 2017

 1. Ghead Grisha (Misri)
 2. Youssef Essrayri (Tunisia)
 3. Janny Sikazwe (Zambia)
 4. Bakary Papa Gassama (Gambia)
 5. Mehdi Abid Charef (Algeria)
 6. Daniel Frazer Bennett (Afrika Kusini)
 7. Eric Arnaud Otogo Castane (Gabon)
 8. Alioum Alioum (Cameroon)
 9. Joshua Bondo (Botswana)
 10. Bamlak Tessema Weyesa (Ethiopia)
 11. Mahamadou Keita (Mali)
 12. Bernard Camille (Seychelles)
 13. Hamada el Moussa Nampiandraza (Madagascar)
 14. Redouane Jiyed (Morocco)
 15. Lemghaifry Bouchaab (Mauritania)
 16. Malang Diedhiou (Senegal)

17 . Denis Dembele (Ivory Coast)

 

——————————————————————-

Mataifa yaliyoshiriki Afcon mara nyingi

 1. Misri (23)
 2. Ivory Coast (22)
 3. Ghana (21)
 4. DRC/Tunisia/Cameroon (18)
 5. Algeria (17)
 6. Morocco (16)
 7. Senegal (14)
 8. Burkina Faso (11)
 9. Mali (10)
 10. Togo (8)

 

——————————————————————-

Makundi

Kundi A:  Gabon, Burkina Faso, Cameroon, na Guinea Bissau.

Kundi B: Algeria, Tunisia, Senegal, na Zimbabwe

Kundi C: Ivory Coast, DR Congo, Morocco, na Togo

Kundi D: Ghana, Mali, Misri, na Uganda.

 

——————————————————————-

Ratiba 

Jan 14

Gabon v Guinea Bissau (Saa 11 Jioni)

Burkina Faso v Cameroon (Saa 2 Usiku)

Jan15

Algeria v Zimbabwe (Saa 11 Jioni)

Tunisia v Senegal (Saa 2 Usiku)

Jan 16

Ivory Coast v Togo (Saa 11 Jioni )

D.R. Congo v Morocco (Saa 2 Usiku)

Jan 17

 

Ghana v Uganda (Saa 11 Jioni)

Mali v Egypt (Saa 2 Usiku)

Jan 18

Gabon v Burkina Faso (Saa 11 Jioni)

Cameroon v Guinea Bissau ( Saa 2 Usiku)

Jan 19

Algeria v Tunisia (Saa 11 Usiku)

Senegal v Zimbabwe (Saa 2 Usiku)

Jan 20

Ivory Coast v D.R. Congo (Saa11 Jioni)

Morocco v Togo (Saa 2 Usiku)

Jan 21

Ghana v Mali (Saa 11 Jioni)

Egypt v Uganda (Saa 2 Usiku)

Jan 22

Cameroon v Gabon (Saa 2 Usiku)

Guinea Bissau v Burkina Faso (Saa 2 Usiku)

Jan 23

Senegal v Algeria (Saa 2 Usiku)

Zimbabwe v Tunisia (Saa 2 Usiku)

Jan 24

Morocco v Ivory Coast (Saa 2 Usiku)

Togo v D.R. Congo (Saa 2 Usiku)

Jan 25

Egypt v Ghana (Saa 2 Usiku)

Uganda v Mali (Saa 2 Usiku)

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU