MURRAY AUMALIZA MWAKA 2016 KWA USHINDI MDOGO, NADAL ANG’ARA

MURRAY AUMALIZA MWAKA 2016 KWA USHINDI MDOGO, NADAL ANG’ARA

365
0
KUSHIRIKI

ABU DHABI, Falme za Kiarabu

NYOTA namba moja duniani katika mchezo wa tenisi upande wa wanaume, Andy Murray, ameukaribisha mwaka 2017 kwa baraka baada ya kupata ushindi wa seti 6-3, 7-6 (6) dhidi ya Milos Raonic na kunyakua nafasi ya tatu katika michuano ya dunia ya Mubadala iliyofanyika jijini Abu Dhabi wikiendi iliyopita.

Murray mwenye umri wa miaka 29, alijitutumua na kupata ushindi huo baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Mbelgiji David Goffin na ushindi huo ulimfanya amalize mwaka na idadi ya michezo 24 ya kushinda.

Bingwa wa michuano hiyo alikuwa ni nyota wa Hispania, Rafa Nadal, aliyemtandika Goffin kwa seti 6-7, 7-6 (7-5).

Muray anasubiri kutetea nafasi yake ya kwanza duniani katika michuano ya wazi ya tenisi ya Australia itakayofanyika katikati ya mwezi Januari.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU