MANE AWAPIGIA GOTI MASHABIKI WA LIVERPOOL

MANE AWAPIGIA GOTI MASHABIKI WA LIVERPOOL

635
0
KUSHIRIKI

MERSESYIDE, Liverpool

MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Sadio Mane, amewaomba msamaha mashabiki wa klabu yake hiyo baada ya kuwazawadia Sunderland nafasi ya kusawazisha bao kwenye mchezo baina yao uliopigwa Stadium of Light.

Majogoo hao wa jiji walianza kufunga kupitia kwa mshambuliaji wao, Daniel Sturridge, kipindi cha kwanza kabla ya Jermain Defoe kusawazisha bao hilo kwa njia ya penalti dakika chache baadaye.

Mane alipachika bao la pili katika dakika ya 70 ya mchezo huo lakini dakika chache baadaye, mshambuliaji huyo wa zamani wa Southampton alijikuta akizuia kwa mkono shuti lililopigwa na mchezaji wa Sunderland huku yeye akiwa ndani ya boksi na ndipo mwamuzi alipoamuru ipigwe penalti iliyowekwa kimiani na Defoe kwa mara nyingine.

Kufuatia sare hiyo ya mabao 2-2 iliyowaacha Liverpool na deni la takribani pointi tano kuwafikia vinara wa ligi Chelsea, Mane aliomba msamaha huo kwa mashabiki kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.

Msenegali huyo alikiri kuwa mwamuzi alikuwa sahihi kuwapa penalti wapinzani wao hao, ingawa alidai kwamba alihisi kusukumwa na mchezaji wa Sunderland kitendo kilichomsababishia majanga hayo ya kushika mpira kwenye eneo la hatari.

“Kusema kweli, mpira ndio uliogusa mkono wangu, kwa sababu kuna mchezaji alinisukuma na nikashindwa kujizuia na mpira ukaupiga mkono wangu.

“Naweza kukubali (kwamba ilikuwa ni penalti). Tunatakiwa kufikiria kuhusu mchezo unaofuata. Tuipokee hii pointi moja,” alisema.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU