MWAKA 2017 UMEANZA VYEMA KWA MURRAY

MWAKA 2017 UMEANZA VYEMA KWA MURRAY

339
0
KUSHIRIKI

DOHA, Qatar

MCHEZA tenisi anayekamata namba moja duniani kwa upande wa wanaume, Andy Murray, ameendeleza wimbi lake la ushindi baada ya kumchapa Mfaransa, Jeremy Chardy, kwa seti 6-0, 7-6 (2) kwenye mchezo wa ufunguzi wa michuano ya wazi ya Qatar Open mapema wiki hii.

Murray mwenye umri wa miaka 29 ambaye hivi karibuni alipewa tuzo ya heshima katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya, alianza mchezo huo kwa kupoteza pointi saba katika seti ya kwanza kabla ya kurudi mchezoni na kumchapa mpinzani wake huyo.

Ushindi huo unaonesha wazi kuwa Murray amedhamiria kunyakua taji la tatu la michuano hiyo ya Doha baada ya kunyakua ile ya mwaka 2008 na 2009 na atakabiliana na Gerald Melzer kwenye mzunguko wa pili.

Murray hajapoteza mchezo wowote wa tangu alipofungwa na Kei Nishikori kwenye robo fainali ya U.S. Open, Septemba mwaka jana. Aliibuka mshindi katika michuano mitano ya 2016 kuanzia hapo na kumshusha Novak Djokovic kwenye nafasi ya kwanza ya viwango vya mchezo huo duniani upande wa wanaume.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU