TAMBWE: KOMBE LA MAPINDUZI LITATUA JANGWANI

TAMBWE: KOMBE LA MAPINDUZI LITATUA JANGWANI

1504
0
KUSHIRIKI
????????????????????????????????????

NA HUSSEIN OMAR

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amissi Tambwe, amesema kutokana na ubora wa kikosi chao watahakikisha Kombe la Mapinduzi litatua katika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Mtaa wa Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA kwa simu kutoka visiwani Zanzibar, Tambwe alisema wamejipanga katika kuhakikisha wanaendelea kufanya vizuri katika mashindano hayo na mengine ya kimataifa.

Tambwe alisema ushindi wanaoendelea kupata katika mashindano hayo ni salamu tosha kwa wapinzani wao wakiwamo Simba ambao leo watacheza na URA kwenye Uwanja wa Amaan.

“Mimi nikwambie kitu, tumejipanga kufanya vizuri zaidi ukilinganisha na misimu mingine na hakuna kitakochoshindikana, licha ya mchezo wa mpira kuwa ni wa matokeo matatu,” alisema Tambwe.

Alisema wachezaji wa Yanga wamejiandaa kisaikolojia kuanzia ndani na nje na hawana wasiwasi wapo tayari kukutana na timu yoyote hata Simba katika hatua ya fainali endapo watafanikiwa kuingia.

“Simba na Yanga ni mchezo ambao hautabiriki, lakini tupo tayari kukutana nao katika hatua yoyote ya michuano hii,  kikubwa ni kwamba sisi tumejipanga kuiwezesha timu kufika mbali zaidi.”

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU