WENGER ADAI HASIRA ZA SANCHEZ NI ZA KAWAIDA

WENGER ADAI HASIRA ZA SANCHEZ NI ZA KAWAIDA

518
0
KUSHIRIKI

LONDON, England


KOCHA Arsene Wenger, amekanusha taarifa kwamba Alexis Sanchez yuko tayari kuondoka kwenye klabu hiyo, baada ya kuonyesha hasira zake hadharani kufuatia sare dhidi ya Bournemouth mwanzoni mwa wiki.

Sanchez hakushangilia pamoja na wenzake bao la kusawazisha kwenye mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya mabao 3-3.

Pia Sanchez alitupa glovu zake chini akionyesha kukasirika kwenye uwanja huo wa Vitality na kudaiwa kwamba aliendelea kutokuwa na furaha hadi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

Lakini Wenger amedai hana tatizo na kile alichofanya nyota huyo wa Chile.

“Kinachoshangaza ni nini? Tunataka kushinda mechi, kama hushindi huwezi kuwa na furaha. Hilo ni jambo la kawaida,” alisema.

“Bila ya hamasa huwezi kutoka nyuma kwa mabao 3-0 dakika ya 70 kisha ukatoka sare. Ni kitu cha kipekee.

“Wote tumechukizwa kama alivyochukizwa Sanchez, ila kila kitu kiko sawa.”

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU