DRAKE ATUNUKIWA TUZO YA UVAAJI BORA, TYGA HAJUI KUVAA

DRAKE ATUNUKIWA TUZO YA UVAAJI BORA, TYGA HAJUI KUVAA

579
0
KUSHIRIKI

LONDON, England


MAPEMA wiki hii rapa Drake ametunukiwa tuzo ya heshima kwa uvaaji bora zaidi duniani upande wa wanaume na tawi la jarida maarufu la G.Q lililopo England huku Tyga akitajwa kuwa mvaaji mbovu wa dunia.

Drake ni ingizo jipya katika orodha ya tuzo ya G.Q ya wavaaji bora 50 duniani mwaka 2017, akichuana vikali na watu wengine maarufu kama Meya wa London, Sadiq Khan na mwigizaji Ryan Gosling.

Marapa wengine walioingia kwenye orodha hiyo ya watupiaji ‘viwalo’ bora ni Tinie Tempah, Pharrell Williams, Jaden Smith na A$AP Rocky.

A$AP Rocky alipata nafasi hiyo baada ya kuanza kujihusisha na masuala ya mitindo hasa alipoanza kuonekana kwenye matangazo ya manukato ya Dior Homme.

Katika orodha nyingine ya mastaa 10 wasiojua kuvaa duniani, Tyga na Nick Cannon walikuwemo.

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU