DEMU WA RONALDO ALIWAHI KUTOKA NA BABU BLATTER

DEMU WA RONALDO ALIWAHI KUTOKA NA BABU BLATTER

864
0
KUSHIRIKI

MADRID, Hispania


MIAKA miwili iliyopita habari iliyokuwa ikitawala vyombo vya habari za michezo ni ile ya mrembo Irina Shayk, ambaye kwa kipindi hicho alikuwa mpenzi wa staa Cristiano Ronaldo.

Siri ilivuja kuwa mrembo huyo aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Sepp Blatter.

Ilikuwa ni bonge la aibu kwa Ronaldo na pia kwa Blatter ambaye kwa kipindi hicho alikuwa kwenye skendo nzito ya kujihusisha na vitendo vya rushwa akiwa Fifa.

Taarifa hizo ziliibuliwa kwa mara ya kwanza na gazeti la El Mundo la nchini Hispania, ambalo lilimtaja Irina kwenye orodha ya mademu waliowahi kutoka na Blatter.

Gazeti hilo lilidai kuwa Blatter ambaye alikuwa na umri wa miaka 79 wakati taarifa hiyo ikitoka, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamitindo huyo raia wa Urusi.

Iliripotiwa kuwa Blatter alizama kwenye penzi la msichana huyo mwaka 2002, baada ya kuvunjika kwa ndoa yake ya muda mfupi na mwanadada Graziella Bianca, ambaye alikuwa shoga wa binti yake.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU