KONTA ATINGA NUSU FAINALI SHENZHEN OPEN

KONTA ATINGA NUSU FAINALI SHENZHEN OPEN

498
0
KUSHIRIKI

BEIJING, China


MKALI wa tenisi upande wa wanawake, Johanna Konta, ameendelea kuonesha ubora wake katika wiki hizi za awali za mwaka 2017 kwa kutinga nusu fainali ya michuano ya wazi ya tenisi ya Shenzhen, baada ya ushindi mgumu dhidi ya Kristyna Pliskova.

Konta ambaye anashikilia nafasi ya kwanza kwa ubora nchini England, alipambana vilivyo dhidi ya mpinzani wake huyo raia wa Czech, ambapo alihakikisha anasahihisha makosa yake ya kupoteza pointi mbili muhimu za seti ya pili na kupata ushindi wa seti 6-4, 6-7 (11-13) na 6-3.

Baada ya ushindi huo na kujihakikishia kucheza nusu fainali, Konta atasubiri mpinzani wake kati ya Katerina Siniakova na Nina Stojanovic, waliotarajiwa kupambana jana kwenye robo fainali ya pili.

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU