MECHI ZITAKAZOAMUA BINGWA BAADA YA CHELSEA KUFUNGWA

MECHI ZITAKAZOAMUA BINGWA BAADA YA CHELSEA KUFUNGWA

1146
0
KUSHIRIKI

LONDON, England


Tottenham wamekatisha ubabe wa Chelsea kwa kuichapa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa White Hart Lane juzi Jumatano usiku na kutoa nafasi kwa timu nyingine kuingia kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England.

Liverpool wana pointi tano nyuma ya kikosi cha Antonio Conte, Chelsea ambao wanaongoza kwa pointi 44, Tottenham wanashika nafasi ya tatu wakiwa sawa na Manchester City kwa pointi 42. Arsenal wakiwa nyuma yao kwa tofauti ya pointi moja, wakati Manchester United wanakuja kwa kasi kwenye kinyang’anyiro hicho wakiwa hawajafungwa mechi 11 za ligi hiyo.

Mtandao umeorodhesha mechi muhimu kati ya timu hizo zinazoshika nafasi sita za juu, ambazo zinaweza zikatoa bingwa wa ligi hiyo.

 

Januari 15: Manchester United vs Liverpool

Liverpool watakuwa wakisaka pointi ili kupunguza pengo dhidi ya vinara Chelsea, watakaposafiri kwenda Old Trafford katika mchezo wao unaofuata wa ligi.

Lakini watakuwa na kazi ngumu baada ya Man United kuanza kuwa kwenye kiwango kizuri. Mchezo wao wa kwanza walitoka sare ya 0-0 kwenye Uwanja wa Anfield, Oktoba mwaka jana.

 

Januari 21: Manchester City vs Tottenham

Spurs ndio waliokuwa wa kwanza kumuonjesha Pep Guardiola kwenye Ligi Kuu England kwa kuwafunga City mabao 2-0 katika Uwanja wa White Hart Lane, Oktoba mwaka jana. Guardiola hatakubali hilo lijirudie tena hasa kwenye uwanja wake wa Etihad.

 

Januari 31: Liverpool vs Chelsea

Hii itakuwa bonge la mechi, itakayosababisha tofauti ya pointi kati ya timu hizo mbili, Klopp atakuwa akisaka ushindi mwingine baada ya kushinda 2-1 kwenye mechi ya kwanza, lakini Conte atakuwa akisaka pointi tatu muhimu ingawa watakuwa kwenye Uwanja wa

Anfield.

 

Februari 4: Chelsea vs Arsenal

Chelsea watakuwa wakihitaji kujiweka sawa baada ya mechi yao dhidi ya Liverpool, wakati watakapowakaribisha Arsenal kwenye Uwanja wa Stamford Bridge. Mechi hizo mbili katika siku tano zitatoa picha yam bio za ubingwa kwa Chelsea.

 

Februari 11: Liverpool vs Tottenham

Mechi zao tatu za Ligi Kuu England za timu hizo mbili zimeishia kwa sare, hivyo kama mechi hiyo itakayopigwa Anfield haitazisaidia timu hizo kama watatoka tena sare.

 

Februari 26: Man City vs Man United

Guardiola na Mourinho watakutana tena, United watataka kurekebisha makosa yao, baada ya mechi ya kwanza kuchapwa mabao 2-1 nyumbani kwao Old Trafford, Septemba mwaka jana.

 

Machi 4: Liverpool vs Arsenal

Mechi ya kwanza ya kufungua ligi ilikuwa kati ya timu hizi mbili Agosti, kikosi cha Klopp kikiibuka na ushindi wa mabao 4-3, lakini safari hii itakuwa ni mechi yao ya 10 kabla ya ligi kumalizika.

Mechi zingine ni za Machi 18 kati ya Manchester City dhidi ya Liverpool, ikifuatiwa ya Aprili 1, ambayo itaikutanisha Arsenal na Manchester City.

Cheslea na Manchester City watakutana Aprili 5, huku Manchester United dhidi ya Chelsea ikiwa ni Aprili 15. Aprili 29 ni Tottenham na Arsenal, kisha Arsenal watakuwa na kazi nyingine dhidi ya Manchester United, Mei 6. Siku sita baadaye Mei 13, Manchester United watakuwa wageni wa Tottenham.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU