UBAGUZI KUWAPONZA MASHABIKI CHELSEA

UBAGUZI KUWAPONZA MASHABIKI CHELSEA

614
0
KUSHIRIKI
SHABIKI

LONDON, England


MASHABIKI wanne wa klabu ya Chelsea wamekumbana na adhabu ya kufungiwa kuingia uwanjani kwa kipindi cha miaka miwili baada ya kukutwa na kosa la ubaguzi wa rangi.

Mashabiki hao wametajwa kumbagua mwenzao mwenye asili ya Kiafrika, tukio lililotokea Februari mwaka 2015, kabla ya timu yao kuvaana na Paris Saint Germain katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kwa mujibu wa taarifa, mahakama kuu ya Ufaransa imetoa adhabu hiyo baada ya kujiridhisha kuwa walitenda kosa hilo wakati Chelsea ilipokuwa jijini Paris.

Sehemu ya video iliyotumika kama ushahidi wa kuwahukumu mashabiki hao, inawaonyesha mashabiki hao wa Stamford Bridge wakiimba: “Sisi ni wabaguzi, sisi ni wabaguzi na ndivyo tunavyopenda.”

Washikaji waliokutwa na msala huo ni Joshua Parsons, James Fairbairn, Richard Barklie na William Simpson.

Mbali na adhabu hiyo ya kutoingia uwanjani, mahakama hiyo ya Ufaransa imewataka kulipa faini ya Euro 10,000 kila mmoja.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU