KOCHA TOTO APIGA HESABU ZA KUKWEPA ‘MKASI’

KOCHA TOTO APIGA HESABU ZA KUKWEPA ‘MKASI’

464
0
KUSHIRIKI

NA JESSCA NANGAWE

KOCHA wa Toto Africans ya Mwanza, Khalfan Ngassa, amesema ataitumia kikamilifu michezo yao mitatu ya nyumbani ili kurudisha matumaini ya kusalia katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Toto Africans ipo katika hati hati ya kushuka daraja kutokana na mwenendo wake wa kusuasua katika ligi hiyo msimu huu.

Akizungumza na BINGWA, Ngassa alisema wataendelea kupambana kwa nguvu ili kuhakikisha wanabakia kwenye ligi na ili azma yao hiyo iweze kutimia watahakikisha wanavuna pointi tatu katika michezo yao mitatu watakayocheza kwenye ardhi ya nyumbani.

“Ni kweli tunahitaji kujituma zaidi kama tunataka kubaki kwenye ligi, tuna michezo mitatu nyumbani ambayo kama tutaitumia vizuri tutafufua matumaini ya kubakia kwenye ligi,” alisema.

Ligi kuu ambayo imesimama kwa sasa kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi, itaendelea hivi karibuni huku Toto ikiwa na michezo mitatu nyumbani dhidi ya African Lyon, Ruvu Shooting pamoja na Prison ya Mbeya.

Toto ipo nafasi ya pili kutoka mkiani ikiwa na pointi 16 juu ya Ruvu Stars inayokamata mkia kwenye msimamo wa ligi kuu.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU