DIAMOND KUWABEBA GABON UFUNGUZI WA AFCON 2017?

DIAMOND KUWABEBA GABON UFUNGUZI WA AFCON 2017?

795
0
KUSHIRIKI

LIBREVILLE, Gabon
SIKU tano zimebaki kabla ya michuano ya Mataifa ya Afrika kuanza Jumamosi hii nchini Gabon na msanii wa Bongo Fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’, atashiriki ufunguzi wa michuano hiyo.

Pamoja na Diamond, msanii mwingine wa Nigeria, Mr Flavour, naye atapamba ufunguzi huo kama walivyofanya kwenye tuzo za mchezaji bora Afrika nchini Nigeria wiki iliyopita.

Baada ya Diamond kufanya onyesho la utangulizi wa michuano hiyo, mechi ya kwanza kati ya wenyeji Gabon na
Guinea – Bissau, itachezwa katika Uwanja wa Port Gentil, kabla ya Cameroon kuumana na Burkina Faso.

Kinara huyo wa muziki nchini Tanzania, ambaye amefanikiwa kubeba tuzo mbalimbali za muziki nchini na barani Afrika atakuwa bora kwa wenyeji hao ambao wanaandaa michuano hiyo itakayoanza Januari 14 hadi Februari 5 mwaka huu?

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU