LUIZIO AMREJESHA MAVUGO ‘FIRST XI’

LUIZIO AMREJESHA MAVUGO ‘FIRST XI’

1295
0
KUSHIRIKI

NA ZAINAB IDDY

JUMA Luizio ni kama ni kama amemrejesha kwenye kikosi cha kwanza mshambultina aliiaji wa Simba raia wa Burundi, Laudit Mavugo, ambaye jana alitikisa nyavu mara mbili baada ya kutofunga kwa muda mrefu.

Mabao mengi ya Simba kwa sasa yamekuwa yakifungwa na viungo huku Mavugo aliyesajiliwa na Simba mwanzoni mwa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, akitokea klabu ya Vital’O, sasa anaonekana si lulu tena Msimbazi licha ya jana kufunga mabao mawili dhidi ya Jang’ombe Boys.

Mavugo huenda akakosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha kocha Joseph Omog, baada ya Juma Luizio, aliyekuwa akicheza katika klabu ya Zesco ya Zambia kuonekana kufaa zaidi kwenye mfumo wa sasa wa Omog.

Luizio aliyesajiliwa katika dirisha dogo la ligi hiyo lililofungwa Desemba 15 mwaka jana, ameanza kuaminiwa na Omog, baada ya kuanza kuonyesha kiwango katika michuano ya Kombe la Mapinduzi ambapo amekuwa mtengenezaji mzuri na mfungaji wa mabao.

Ujio wa Luizio katika kikosi hicho unaonekana kuleta ushindani katika nafasi ya ushambuliaji inayoundwa na Fredrick Blagnon na Mavugo ambao wawili hao bado hawajaonyesha uwezo mkubwa wa kufunga mabao.

Luizio anayecheza Simba kwa  mkopo ameonyesha kiwango cha hali ya juu katika michuano ya Kombe la Mapinduzi na kuiwezesha timu yake hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Taifa Jang’ombe, huku akitupia moja, lakini akiwa chachu ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KVZ ya Zanzibar.

Mshambuliaji huyo ameonyesha uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, kupokea pasi na kupiga mashuti jambo lililoonekana kumvutia Omog na kuendelea kumpa nafasi katika kikosi chake.

Akizungumza na BINGWA, Luizio amesema michuano ya Kombe la Mapinduzi anayatumia kama sehemu ya kujiweka fiti  kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara.

Luizio alisema anashukuru kwa kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha Omog, kwani ataendelea kuonyesha kiwango ili waweze kufanya vizuri.

Jana Luizio alikuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya Jang’ombe Boys ambapo alitengeneza bao la kwanza kwa kutoa pasi safi kwa Shiza Kichuya ambaye lipiga shuti lililogonga mwamba kisha kumkuta Mavugo aliyeukwamisha kimiani na kuiandikia Simba bao na kuongoza katika mchezo huo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU