STAND UNITED WAWAPIGIA GOTI WACHEZAJI

STAND UNITED WAWAPIGIA GOTI WACHEZAJI

440
0
KUSHIRIKI

NA ZAINAB IDDY

UONGOZI wa Stand United  inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, umeamua kuwapigia goti wachezaji wao,  baada ya kuwataka kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu wanachokabiliwa na ukata.

Klabu hiyo kwa sasa inakabiliwa na hali ngumu ya kifedha baada ya Kampuni ya Acacia kusitisha mkataba wa kuidhamini kutokana na mgogoro ulioibuka mwaka jana baina ya makundi mawili ya wanachama wao.

Akizungumza na BINGWA jana Ofisa habari wa klabu hiyo, Deo Makomba, alisema wachezaji wao wanatakiwa  kuwavumilia kwani wanafahamu  kuna baadhi yao wanadai fedha zao za  usajili.

Makomba alisema wanaendelea kutafuta  mdhamini mwingine ambaye ataweza kuisaidia klabu hiyo ili waweze kufanya vizuri katika michezo yao ya Ligi Kuu Bara.

“Tunafahamu kuna baadhi ya wachezaji wanatudai fedha za usajili, kuna mchakato unaendelea kufanywa na viongozi kumpata mdhamini mpya, lakini pia wapo wadau wa soka Mkoa wa Shinyanga tunazungumza nao kwa lengo la kuweka masuala sawa.

“Kiukweli kwa sasa Stand United tumeyumba kifedha, tunategemea udhamini Vodacom na Azam, lakini siku si nyingi mambo yatakaa sawa na tutalipa wachezaji wetu,” alisema.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU