STRAIKA SIMBA ATABIRIWA MAKUBWA

STRAIKA SIMBA ATABIRIWA MAKUBWA

1455
0
KUSHIRIKI

NA WINFRIDA MTOI

KOCHA wa zamani wa Pastory Athanas, Muhibu Kanu, amesema straika huyo mpya wa Simba, akizoea mazingira na  mfumo wa Joseph Omog, atakuwa hashikiki katika kikosi hicho kwani atatupia sana mabao katika msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Athanas aliyesajiliwa na Simba katika dirisha dogo la Ligi Kuu Tanzania Bara lililofungwa Desemba 15 mwaka jana akitokea Stand United, ameanza kuaminiwa katika kikisi cha Omog kutokana na uwezo wake.

Akizungumza na BINGWA jana, Kanu alisema anafahamu vizuri uwezo wa straika huyo, kwani aliwahi kumfundisha wakati akiwa na timu ya vijana ya Toto Africans.

Kanu alisema ni moja ya washambuliaji wenye uwezo mkubwa wa  kufunga mabao na akizoea mfumo wa Omog  tatizo la ukame wa mabao Simba litaondoka.

“Mimi kama kocha naweza kusema, Pastory Athanas ni mchezaji mwenye kipaji cha asili, ninafamu uwezo wake tangu nilipokuwa naye Toto Africans na baadaye Stand United, ni mchezaji anayejituma,” alisema Kanu.

Alisema kinachotakiwa kwa sasa ni kupewa muda wa kuelewana na wachezaji wenzake wa Simba kwa kuwa hakuwepo kipindi cha maandalizi ya msimu mpya.

“Unaweza ukamwona mchezaji wa kawaida kwa kuwa bado hajaelewana na wenzake vizuri, lakini naamini Simba walifanya chaguo sahihi kumchukua,” alisema Kanu.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU