SURE BOY: YANGA ILITUDHARAU

SURE BOY: YANGA ILITUDHARAU

888
0
KUSHIRIKI

NA ZAINAB IDDY

KIUNGO mshambuliaji wa Azam, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, amesema Yanga walidharau uwezo wao kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea kwenye Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar.

Akizungumza na BINGWA jana kwa simu kutoka Zanzibar, Sure Boy,  alisema dharau zao ziliwaponza na kujikuta wakifungwa na wao mabao 4-0 katika mchezo wa makundi uliochezwa juzi usiku kwenye uwanja huo.

Sure Boy alisema Yanga waliwachukulia  kawaida wakiamini wangeweza kuibuka na ushindi kama  ilivyokuwa katika michezo ya awali dhidi ya Jamhuri ya Pemba ambao walifungwa mabao 6-0 na kisha bao 2-0 dhidi ya Zimamoto.

“Wamesahau kuwa sisi tunawajua na wote tunacheza soka la Tanzania Bara, tunashukuru Mungu kuondoka na ushindi, lakini walistahili tuwafunge zaidi ya bao zile ili kuwaonyesha Azam si timu ya mchezo mchezo pale inapotaka kufanya jambo lake,” alisema.

Kwa matokeo hayo Azam imefikisha pointi saba ikiongoza Kundi B ikifuatiwa na Yanga wenye pointi 6.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU