TUZO YA MCHEZAJI BORA KUMSAIDIA MAHREZ KUBEBA TAJI AFCON 2017?

TUZO YA MCHEZAJI BORA KUMSAIDIA MAHREZ KUBEBA TAJI AFCON 2017?

407
0
KUSHIRIKI

LIBREVILLE, Gabon

WINGA wa timu ya taifa ya soka ya Algeria, Riyad Mahrez, amesema shabaha yake kwa sasa ni kuisaidia timu yake hiyo kunyakua taji la Afcon mwaka huu baada ya kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa Afrika akiwapiku Pierre-Emerick Aubameyang na Sadio Mane.

Mahrez aliisaidia klabu yake ya Leicester City kunyakua taji la Ligi Kuu England msimu uliopita na amekiri kuwa hataridhika nayo hivyo amedhamiria kuisaidia timu yake kunyakua taji la michuano ya Afrika itakayoanza kutimua vumbi mwezi huu nchini Gabon.

“Nina furaha kunyakua tuzo hii ambayo nilikuwa naiwania na wachezaji wengine wawili wazuri mno. Haikuwa rahisi hivyo nimefurahishwa nayo na nitaendelea kupambana.

“Kitu kingine baada ya hii tuzo ni kuhakikisha Algeria tunakuwa mabingwa wa Afcon mwaka huu. Tutajaribu kufanya makubwa hapa (Gabon).

“Haitakuwa kazi nyepesi lakini itakuwa jambo jema iwapo tutashinda,” alisema.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU