YANGA YAMPA JEURI STRAIKA AZAM

YANGA YAMPA JEURI STRAIKA AZAM

1069
0
KUSHIRIKI
????????????????????????????????????

NA SALMA MPELI

STRAIKA wa Azam, Joseph Mahundi, amefungua akaunti ya mabao kwenye timu yake hiyo mpya, baada ya juzi usiku  kuifungia bao moja kati ya ushindi wa mabao 4-0 walioupata dhidi ya Yanga kwenye Kombe la Mapinduzi na kusema kuwa ataendelea kufunga hadi kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezaji huyo aliyesajiliwa na Azam kwenye usajili wa dirisha dogo hivi karibuni akitokea Mbeya City, katika mchezo huo dhidi ya Yanga alifunga bonge la bao kwa shuti la mbali.

Akizungumza na BINGWA jana kwa simu kutoka Zanzibar, Mahundi alisema ataendelea kufunga kadiri atakavyopata nafasi katika michuano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.

Mahundi alisema baada ya mashindano hayo atahamishia makali yake Ligi Kuu Bara.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU